Kujibu maombi ya picha

Tafakari vyema kabla ya kutuma picha!

Nilikutana na msichana/mvulana nikampenda na sasa ananiomba nimtumie picha yangu. Sina uhakika kama kufanya hivyo ni jambo jema…?

  • Zingatia kwamba utakapokuwa umemtumia mtu picha au video - ya aina yoyote ile – hutaweza tena kudhibiti jambo lolote litakalofanyiwa vitu hivyo. Picha au video vinaweza kusambaa kwa kasi ya ajabu katika intaneti.
  • Unaweza kumuamini huyo mtu lakini endapo kwa bahati mbaya uhusiano wenu ukivunjika , au mkigombana au kama simu yako itaibiwa , picha au video uliyotuma vinaweza kutumiwa kukubughudhi au kukufanyia mambo ya kukuumiza.
  • Ni vigumu sana kuondoa picha/video katika intaneti baada ya kusambazwa.
  • Usifanye jambo ambalo utajalijutia.

Kidokezo cha intaneti kinachofuata:

Précédent Suivant

Average Rating: (0 reviews)

Leave Your Feedback

Recent Reviews

Notifications