Dalili za ugonjwa wa Ebola ni zipi?
Dalili za ugonjwa wa Ebola uanza kujitokeza kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi. Mgonjwa wa Ebola huwa na dalili zifuatazo:
- Homa kali ya ghafla
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu ya mwili, misuli na viungo
- Kuharisha (kunaweza kuambatana na damu)
- Kutapika (kunaweza kuambatana na damu)
- Vipele mwilini
- Kuvia damu chini ya ngozi au kutokwa na damu puani, mdomoni, machoni, na masikioni na sehemu ya haja ndogo na kubwa
Makala Inayofuata
Average Rating: ☆ ☆ ☆ ☆ ☆ (0 reviews)