Nani wapo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa ebola?
Kila mtu yupo katika hatari ya kuambukizwa na virusi vya ebola, hata hivyo makundi ya watu wafuatao wapo kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya ebola:
- Wanafamilia, majirani na marafiki wanaoishi na/au kumhudumia mgonjwa wa Ebola
- Waombolezaji ambao wanaweza kugusa mwili wa marehemu kama sehemu ya utaratibu wa mazishi
- Watu wanofanya kazi ya kuhudumia watu wengi - hospitali, benki, vitengo vya huduma kwa wateja kwenye taasisi mbali mbali, wasafishaji n.k
- Wawindaji wa msituni ambao wanaweza kugusa mizoga ya wanyama
Makala Inayofuata
Average Rating: ☆ ☆ ☆ ☆ ☆ (0 reviews)